Makala
MAKUBWA MATATU YANAYOKUJA MACHO YA MOYO WA MTU YANAPOTIWA NURU
| Makala
Waefeso:1.18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
1. TUMAINI LA MWITO WAKE-Kwamba lipo TUMAINI LA WITO au KUITWA au MWITO ambalo mtu hulijua akishatiwa NURU ndani ya ufahamu wake. Kila mtu aliyeokoka anatakiwa kuwa na kujua kuwa tumeitwa kwa tumaini linaitwa BLESSED HOPE....kwamba si tu katika wakati huu wa sasa bali zaidi sana katika wakati waa umilele ujao...hatuchoki kwani tunajua tumeitwa na aliyetuita ni Mungu....kila aliyeitwa anajua lipo kusudi la kuitwa kwake....anaishi akiwa amejaa SHAUKU akijua kuwa mwisho wa siku upo utukufu mkubwa zaidi ya mateso tunayopitia leo.
Mfano: Ni kama leo upokee simu kuwa unaitwa na rais na unatakiwa kusafiri kesho....haha hahaha wengine hawatalala, utaahirisha kila kitu ili ULE WITO uwe na thamani kwako....hutakubali kikwazo chochote kiingilie kati WITO huo....ndio biblia inasema hapa duniani sisi ni wapitaji,wenyeji wetu uko mbinguni....tumeitwa jamani....
Lazima. Mateso ya imani yako kwake....Warumi 5:3
Blessed Hope!
2 Wakorintho 4:16-17
16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
2. UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI-Macho ya moyo yakitiwa nuru ni lazima ujue kuwa kwanza WEWE NI URITHI KWA MUNGU na pili ujue kwamba MUNGU ANAO URITHI KWA AJILI YA WATATKATIFU au watoto wake...mahali pengine biblia inasema SISI NI WARITHI PAMOJA NA KRISTO...hii inakupa picha kwamba upande uliopo sio masikini....vipo vitu vya kurithi...tena urithi wa milele...ila kabla hatujarithi mwishoni tunatumia sasa vile ambavyo Baba yetu wa mbinguni ametupa. Sisi ni matajiri, sisi ni wakwasi....sio tu wa mali za mwilini bali zaidi sana wa siri za ufalme wa Mungu.
Jambo la tatu linapatikana msitari wa 19....ulete hapa
Ukisoma vizuri NENO LA MUNGU utagundua kuwa mambo mengi tunajitakia wenyewe kwa ujinga na ulimbukeni wetu....
Hakika Utajiri ni haki yetu tatizo ni upofu wa rohoni tu.
Waefeso 1:3
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Waefeso 1 :6
6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Waefeso:1.19
na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;
3. UBORA WA UKUU WA UWEZA-Hapa unaona kabisa kuwa UKUU WA MUNGU ni wa kiwango cha mwisho na cha juu kabisa kwa ubora...na huu uweza wake unafanya kazi ndani yetu tuaminio kwa kadri ya utendaji wa nguvu zake. Kumbuka hapa inaonyesha wazi kuwa nguvu za Mungu zinafanya kazi ndani yetu...Angalia Efeso 3:20 uunganishe hapa....kizuri na cha kufurahisha na kutia moyo ni kwamba hizi nguvu ndo zile zile zilizomfufua Yesu Kristo toka kwa wafu....wow wow
Waefeso:3.20
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Nguvu za Mungu zinafanya kazi kwenye maisha yetu kwa kutegemea namna ambavyo hizo nguvu ziko hai ndani yetu. Kama una nguvu za Mungu kiwango cha kijiko huwezi kupata matokea ya maombi kiwango cha pipa hata kama umeomba masaa mia nane tisini.
So mpaka hapo umeona hayo mambo matatu makubwa?????????????
Ufahamu sahihi una nguvu sana.
Tumalizie leo na Warumi 1:28 na Hosea 4:6....twende
Warumi:1.28
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Hosea:4.6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
SADAKA